Je Mungu ana nia mbili?

Na: David Sterling
Kutoka: December 2008
Patikana ndani ya: Lakale kushindana na agano jipya
Je Mungu wakati mwingine hupenda na kuchukia, wakati mwingine huonyesha gadhabu na wakati mwingine huonyesha rehema? Ni nini kime sababisha huu mchafuko kuhusu Mungu na utendaji wake kwa mwanadamu?

Mungu ni Mungu mwema! Yeye hatukasirikii sisi! Yeye hatupendi tu,ila anatufurahia sisi.Yeye hatawahi kutuacha wala kututupu sisi, haijalishi tume shindwa kiasi gani, kukosea kiasi gani. Makosa yetu hayamsababisha yeye kuzuia baraka Zake! Utendaji wetu uliyo duni na makosa yetu hayabatilishi tabia Yake kuelekea sisi! Kuu ni uaminisfu Wake!

Hizi ni semi zilizo na nguvu na asili. Bahati mbaya, hazi sikiki sana mara nyingi, hata katika mizururo za kikristo. Epu fikiria kuhusu yale mafundisho ya asili ambayo tuna sikia kila wakati kuhusu asili ya “kweli” ya Mungu:
- Mara nyingi Mungu anaonekana kama mwenye hasira na akiwa tayari kutushika katika kushindwa kwetu na makosa yetu. Yeye anatuangalia kuona jinsi tunavyo tenda sasa, tangu tuwe watoto Wake. Hakika hawezi jibu maombi yetu iwapo tume tenda dhambi,na ata zuia baraka Zake iwapo hatuenendi na makadario yake. Hakuna hatua ya kutarajia kibali cha Mungu bila mtu kuishi maisha yasiyo na lawama.

Haya mawazo kuhusu asili ya Mungu yana ongoza vibaya; huongoza katika mwisho mbaya kuhusu asili ya Mungu na tena inayo zuia uhusiano wa karibu na Mungu .Huu ni utandaji ulio juu ya mzingi ya Sheria, dini ndilo zuio kuu kwa kupata uzoefu wa uhusiano unao ridhisha Baba wetu wa mbinguni.

Kuchanganya Agano la Kale and Agano Jipya imeleta machafuko kwake Mungu na utendaji wake kwa mwanadamu.

Kwa nini anathirishwa katika namna hiyo?

Jinsi gani watu walio hakika wamekuja katika mwisho huu kuhusu asili ya Mungu? Kwa nini inawezekana ya kwamba Mungu anaonekana sana ikitukirimia kwa kadri ya tabia njema na utandaji? Jawabu la maswali ya aina hii inaweza patikana katika kukosa kuelewa umoja kati ya Agano la Kale na agano Jipya. Kuto elewa sawa sawa umuhimu na maana ya kazi ya ukombozi yaYesu ime sababisha waumini mara nyingi kueleza Mungu vibaya. Kuchanganya Agano la Kale na Agano Jipya ina zalisha mchafuko kuhusu utendaji wa Mungu na mwanadamu.

Mungu amethibitisha kwa mifano kutoka Agano la Kale

Katika Agano la Kale, Mungu mara nyingi alionyesha gadhabu na hukumu Yake katika njia ya uharibifu.Tuna mifano nyingi za ukali ambako Mungu alihukumu nazo dhambi na akamwaga gadhabu Yake juu ya mataifa na watu kibinafsi:
- Mapema sana katika historia ya mwanadamu tulikuwa na garika la Nuhu, ambako watu nane wa waliokolewa na maangamizo yakatendeka.
- Tuna ona uharibifu wa Sodomu na Gomorah ambalo Bwana wetu Yesu aliweza kulitaja katika mafundisho.
- Malaika wa mauti aliwaua watoto wa kifungua mimba watu na ikasababisha maangamizo makuu katika usiku moja huko Misiri.
- Malaika mwingine akaua maskari 185,000 wa Ashuru usiku moja.
- Viongozi waasi waliangamizwa katika makabila Israel kama mfano mkuu wa wengine.

Kwa hivyo hii nakala ina endelea na kuendelea. Hakuna shaka ya kwamba Mungu ni Mungu mtakatifu ambaye bila shaka ana chukia dhambi na hutaka haki. Ndiyo, Mungu wakati mwingine, alikuwa na hasira sana katika agano la Kale. Kuna mifano nyingi zilizo nakiliwa za gadhabu kubwa na hukumu ya upesi. Mtume Paulo anatuambia ya kwamba kila kitu kilicho andikwa katika Agano la Kale ni mfano kwetu sisi (1 Wakorintho 10:11).

Mungu jinsi anavyo funuliwa na Yesu

Walakini, kuna pia kufunuliwa kwa Mungu ambako Yesu alionyesha kupitia matendo Yake na mafundisho. Yesu alisema ya kwamba yule aliye mwona Yeye amemwona Baba. Alionyesha rehema kwa watenda dhambi wakuu na msamaha wa haraka na urejeshi. Tendo lake la mwisho la kutufilia dhambi zetu, lili thibitisha bila shaka Alikuja kuokoa ulimwingu na sio kuhukumu . Umebadilishwa sana na kuja kwake Yesu! Agano la Kale la Sheria, ambayo ilikuwa huduma wa kifo, imepita mbali sasa! Sisi tuna ishi nyakati zilizo tofauti, chini ya agano jipia lilo kamamilifu!

Je Mungu ana nia mbili?

Je ni vipi picha ya Mungu ambayo Yesu alifunua inaingiane na mtizamo wa Agano la Kale uliokuwa kali na uzito wa Mungu? Je Mungu amebadilika ? Mungu ni jizi? Je wakati mwingine Yeye anatupenda na wakati mwingine ana tuchukia sisi? Je ni vipi tunaweza kuusaina na Mungu ambaye hali yake ina onekana inabadilika mara kwa mara kutoka kipeo kimoja hadi kingine.

Haya aina ya maswali huleta mshangao ambao umewafanya watu wengi kuwa katika hali ya shaka na hofu. Watu walio hakika wengi wamechanganyikiwa kwa sababu ya ishara nyingi zilizo changanywa ambazo zimetumwa kwao na kanisa na walimu wake.

Kuna asili moja ya Mungu iliyo kweli na ambayo ime wakilishwa katika Neno na ni UPENDO!

Kuna jawabu rahisi kwa maswali haya na umoja kati ya gadhabu ya Mungu and rehema ya Mungu. Mungu hana nia mbili! Kuna asili moja ya Mungu ya kweli ambayo imewakilishwa katika Neno na ni UPENDO! 1Yohana 4:8 ina sema, “Mungu ni pendo” Na Yeye hatupendi tu wakati fulani - UPENDO ndiye asili ya Mungu! UPENDO ni asili Yake isiyo badilika na iliyo ya kudumu. Yesu anatoa mfano ulio wazi wa Mungu aliye kweli.

Masharti ya utakatifu inaohitajika kwa haki sasa imredhishwa

Mungu, ni mtakatifu aliweka dhambi zetu na dhambi za ulimwengu wote juu yake Yesu, na Akamwadhibu kwa niaba yetu. Msalaba ambao Yesu alitolewa dhabihu kama mwana kondo wa Mungu asiye na ua umebadilisha uhusiano wa mwanadamu kuelekea Mungu. Kunayo tafauti kati ya vile Mungu alikabiliana na mwanadamu ndani ya agano la Kale na jinsi sasa anakabiliana na mwanadamu chini ya Agano Jipya. Malipo ya Yesu kwa dhambi zetu hata milele ilibadilisha uhusiano wetu na Baba. Mungu mwenyewe hacha badilika hata kidogo, lakini aliridhishwa masharti Yake matakatifu ya haki kwa kumwadhibu ya Yesu kwa niaba yetu. Hii haikuwa malipo nusu ambayo ingehitaji sisi kuongezea utakatifu wetu na utendaji wa kidini - ilikuwa ni malipo kamili na ya mwisho, ambayo ina tuwacha bila kitu kingine ila ni kuamini na kupokea. Kwa uhakika hakuna kitu tunaweza kufanya kubadilisha upendo wa Mungu kutuelekea sisi!

Kabla ya dhabihu ya Yesu hukumu kuu ili letwa juu ya mwanadamu. Kabla Yesu atimilize matakwa matakatifu na kufa kwa niaba yetu. Mungu alilazimika kuadhibu dhambi. Hii haikuwa kwamba Bwana alitamani kuadhibu. Upendo wake kila wakati umekuwa upendo uliyopo.Walakini, gharama ilipaswa kulipwa kwa ajili ya uasi na dhambi za mwanadamu, mpaka hiyo sadaka ilitolewa, tulikuwao na matokeo ya dhambi.

Kabla Yesu aje, kulikuwa na gadhabu toka kwa Mungu juu ya mwanadamu kwa ajili ya dhambi zake. Sheria ya Agano la Kale ilikuwa ni huduma wa gadhabu. Dhambi za watu zilikuwa juu yao. Lakini wakati Yesu alipo kuja, Mungu alikoma kushikilia dhambi za watu juu yao. Hii ndiyo mtume Paulo anatangaza katika 2 Wakori.5:19,21.

Upatanishi na amani

Neno “upatanishi” linazungumza kuhusu kutengeza amani. Mungu tena hatuwekei sisi kuwajibika tena, badala yake Aliweka dhambi zetu juu ya Yesu. Akimfanya Yesu kuwajibika kwa ajili ya dhambi zetu.Yesu akawa sisi ili tuwe jinsi yeye Alivyo - yaani haki ya Mungu. Mungu hayupo katika vita na mwanadamu tena kwa sababu Sadaka ya Yesu alimaliza hizo vita - na sasa tuna ishi kwa amani na Mungu kupitia kifo cha Yesu ( Warumi 5:1).

Yeye hawapi nyinyi yale mwapaswa kupata ila Yeye anawapi yale Yesu anapaswa kupata!

Mungu sifiwe - Yeye hawapi nyinyi yale mnapaswa kupata ila Yeye ana wapa yale Yesu anapaswa kupata ! Yesu amebeba gadhabu ya Mungu yote na sasa tuna ishi chini ya Agano Jipya katika majira ya neema na kibali cha Mungu. Mungu hajakasirika na hangojee nafasi ili amwage gadhabu Yake juu yako iwapo unaweza kufanya makosa.

Mungu anakupenda licha ya wewe kutokuwa makamilifu hata ndani yako mwenyewe. Hakupendi sio kwa kutenda kwako lakini kwa sababu ya Sadaka ya Yesu.Wewe peleka mizizi na kuwa uthabiti katika Upendo na neema ya Mungu! Jitambulishe na kikamilifu kwa Agano Jipya na ufurahie faida zote kama kiumbe kipya katika Kristo.Wewe umependwa na kukubalika kwa sababu ya yale Yesu amefanya - iliyo kinyume cha kutenda kwako mwenyewe na usitahili wako. Kustahili kwa Yesu ni safi na Yesu mwenywe ni zaidi ya tosha! Mungu kwa ukamilifu ameridhika na Yesu - wewe pia unaweza kuridhika na yale Ametenda!

Na: David Sterling

Pastor of Tampereen Kristillinen Yhteisö, Finland. Member of GGN Board of Directors

Mengi Kuhusu David Sterling | Nakala iliyoandikwa na David Sterling