Kufunuwa Yesu kwa watu wa mataifa imekuwa pigo la moyo. Mke wangu na mimi na vijana wetu watatu tumekuwa wamishonari kule Ufilipino kwa miaka 9.
Tumekuwa na tunuko la kusaidia kuanzisha kanisa, na kusimamia jumba la watoto yatima, tumefundisha katika Shule za Bibilia na kusafiri katika matifa mengi ya Ashia Kusini.
Miaka mitatu zilizo pita tulikuwa tuna waza kuhusu kufunga mizigo zetu na kurejerea Amerika. Lakini Mungu bado hakuwa amemaliza na sisi. Nafasi ya hudumu mpya ikafunguka na tukaenda katika mji mkubwa wa Manila. Wakati huu wa mabadiliko rafiki yangu mshonari alianza kutupa kanda, nakala za mafundisho kuhusu soma la neema. Sikuwa na jambo lolote hapa mwanzoni jinsi maisha na huduma wangu ungeweza kupata mabaliko makubwa. Ufunuo wa neema na wema wa Mungu ulibadilisha mtembeo wangu ndani yake kuingia katika maisha ya uhusiano wa kujitolea kwa Mungu mpenzi. Nime tambua ya kwamba chochote nitendacho ni katika mjibu wa yale Amesha nifanyia mimi. Nina penda nuku hii ya Watchman Nee : “Ukristo hauanzi na kwa kutenda makubwa,ila unaanza na makubwa ambayo yamesha tendwa.” Ni wakati tu nilipo anza kutizama kwa yale Kristo alisha fanya ndipo nalitambua ya kwamba nina nguvu na uweza wa kufanya kazi za Kristo.
Miaka ya kujaribu kufanya kitu kutendeka katika huduma wangu yalikuwa yamenifanya mimi kuchoka na kusumbukana. Huu muktadha toka Mathayo 11:28-30 katika ujumbe wa Bibilia ilifunguwa macho yangu kwa njia ajabu aliyo ya maisha mapya : “Je umechoka? Umeisha? umechoka katika dini? Njoo kwangu. Jiunge nami na utarejesha maisha yako. Nitakuonyesha jinsi ya kupata pumziko. Tembea na fanya kazi na mimi- angalia jinsi ninanvyo fanya. Jifunze mitundo zizo lazimishwa za neema. Sita weka kitu chochote mzito au kibaya juu yako. Jiunge na mimi na utajifunza kwa wepesi na huru.
Na sio tu “mitundo zizolazimishwa za neema” zilirejesha furaha yangu, ila imenifanya kuwa mtu wa kuzalisha katika huduma wangu. Kokote niendako napata watu walio katika mashua nilikokuwa, nikifanya kazi kwa bidii lakini ninatimiliza kidogo,nimechoka na kuishi katika dini. Na tena nime tambua ya kwamba ukiendele kuangalia kazi ya Kristo iliyokamilika, watu wata itikia katika umati. Ni la ajabu ambalo Mungu atatenda ndani yako unapo weza kufunuwa Yesu na yale Amefanya. Ukifanya kuwa rahisi watu kupokea na kuangalia. kwake Kristo na yale amefanya yanachochea njaa ndani ya watu na kufanya kuwa rahisi kupokea chochote wanahitaji tiko kwa Mungu. Imani kwa yasio ya kawaida yana kuwa hai tunapo toa macho yetu kujiangalia wenyewe na kuangalia kwake Kristo, mwanzilishi na mkamilishi wa Imani yetu.
“Ufunuo wa neema na wema wa Mungu ili badilisha mtembeo wangu ndani yake kuwa maisha yanayo toa uhusiano na Mungu anipendeye. ”
Nilifikiri kwamba kusudi kuu maishani mwangu ni kuiga matendo ya Kristo. Kama Wakristo wengi wamuhimu kilio cha vita vyangu kilikuwa “ Je Yesu atafanya nini” Nimetambua ya kwamba sija itwa kuiga Kristo, ila ni kuishi katika Kristo. Kwa sababu ya neema ya Mungu sisi sio waigaji au watizamaji- la, sisi ni washirika (Wakol 1:12). Tuna weza kuingia ndani ya yale yote Kristo ametizimiliza kwa ajili yetu.
Ujumbe mwingine wa neema ni kuongezeka katika ujasiri. Waebrania 10:19 inasema “Basi, ndugu, kwa damu ya Yesu tunapewa moyo thabiti wa kuingia Mahali Patakatifu.” Nina ona na kuelewa kuliko awali kwa sababu ya dhabihu ya Yesu, hakuna kitakacho nizuia kuingia weponi mwa Mungu. Nina kata kuruhusu hatia na hukumu ya makosa ya mambo yaliyo pita kunizuia kutembea katika mpango wa Mungu. Sasa nina jua, Yesu alihukumiwa ili niwe huru na mwepesi.
Nime ona katika nafasi ya kwanza vile dini inajaribu kuzuia wewe kufika weponi mwa Mungu katika kufanya wewe kuangalia yale unahitaji kufanya. Huwa nalia wakati watu wananiambia maishani mwao mwote wamejihizi kutostahili au wao si wazuri sana kuwa na uhusiano na Mungu. Je ni furaha gani kuambia hawa watu kwamba Mungu anawakubali wote na sio kadri ya yale wamefanya,ila yale Yesu tayari ametimiliza kwa ajili yao.
Nime tambua tena Bibilia inakuwa hai kuliko awali unapo mtafuta Yesu. Yeye ndiye kamba nyekundu inayoanza katika katika Kitabu cha Mwanzo hadi Ufunuo wa Yohana. Neema imefungua macho yangu kumuona Yeye kuliko awali, na sio tukumwona Yeye ila kuingia katika uzima Wake. Huu ndiwo wito wangu kama mhuduma wa Injili- kuruhusu watu wajue ya kwamba mitego zimeondolewa na ni wakati wakuingia ndani. Je ni furaha gani kuibiri habari njema !
Huyu mwandishi anatoka Amerika, lakini jina lake haliwezi kujulikana kwa sababu ya hali iliyopo katika mataifa mojawapo yeye na jamii yake wanahudumu ndani.
- Barua ya Mwandishi
Nakala zinaweza kuipigwa chapa mradi zina chapishwa katika
ukuu wake wote na pongezi zitolewe kwa to Global Grace News http://www.globalgracenews.org.